Wala usipokee kutoka kwa wageni nyama wa namna hiyo na kunitolea mimi Mungu wako kama chakula. Nyama hao wana kilema kwa vile wamekatwa na hawatakubaliwa kwa faida yenu.
Ngombe dume, kondoo dume au beberu akizaliwa atabaki na mama yake kwa siku saba. Lakini tangu siku ya nane anaweza kutolewa kwa Yawe kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto.