Musa akamwambia Haruni na wana wake waliobakia, Eleazari na Itamari: Mutwae ile sehemu ya sadaka ya vyakula iliyobakia kutoka sadaka Yawe anazotolewa kwa moto. Muikule karibu na mazabahu bila kutiwa chachu kwa sababu ni takatifu kabisa.
Kwa nini hamukumukula katika Pahali Patakatifu kwa vile huyo ni kitu kitakatifu kabisa na mulikuwa mumepewa huyo kwa kuondoa kosa ya Waisraeli wote pamoja na kuwafanyia ibada ya upatanisho mbele ya Yawe?
Kisha atachinja yule mwana-kondoo katika Pahali Patakatifu, wanapochinjia nyama wa sadaka kwa ajili ya zambi na sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Sadaka hii kwa ajili ya kosa na vilevile sadaka kwa ajili ya zambi, ni mali ya kuhani. Ni sadaka takatifu kabisa.
Wala usipokee kutoka kwa wageni nyama wa namna hiyo na kunitolea mimi Mungu wako kama chakula. Nyama hao wana kilema kwa vile wamekatwa na hawatakubaliwa kwa faida yenu.
Lakini kitu chochote kilichotakaswa kwa Yawe, kama ni mutu au nyama au kitu kilichopatikana kwa urizi, hakitauzishwa wala kukombolewa. Chochote kilichotakaswa kwa Yawe ni kitakatifu kabisa.
Usipikwe hata kidogo pamoja na chachu. Nimewapa wao sehemu hiyo kutoka sadaka wanazonitolea kwa moto. Ni sadaka takatifu kabisa kama vile sadaka kwa ajili ya zambi na kwa ajili ya kosa zinavyokuwa.
Ninakupa wewe, wana wako na wabinti zako, vitu vyote ambavyo watu wa Israeli wananitolea; hivyo ni haki yenu siku zote. Hili ni agano la milele mbele yangu ambalo ni kwa ajili yako na wazao wako.
Munajua hakika kuwa wale wanaotumika katika hekalu wanapata chakula chao ndani ya hekalu. Na wale wanaotumika kwa kutoa sadaka juu ya mazabahu wanapata sehemu yao kutoka sadaka zile.