Halafu, bila kujua kwamba huyo alikuwa muke wa mwana wake, akamwendea pale kando ya njia, akamwambia: “Ninataka kulala nawe.” Tamari akamwuliza: “Utanipa nini upate kulala nami?”
Yuda akamwuliza: “Unataka nikupe nini kama rehani?” Naye akamujibu: “Unipe hiyo pete na kamba yake pamoja na hiyo fimbo unayoshika.” Basi, Yuda akamupa vitu hivyo vyote, akalala naye. Tamari akapata mimba yake.
Lakini mwizi akishikwa wakati jua limechomoza na kuuawa, aliyemwua atakuwa na kosa. Mwizi anapaswa kulipa. Ikiwa hana kitu cha kulipa, basi, yeye mwenyewe atauzishwa kwa kulipa kile alichoiba.