5 Ikiwa sadaka unayotoa ni ya mukate uliokaangwa kwenye kikaango, hiyo itakuwa ya unga laini uliochanganywa na mafuta ya zeituni lakini bila chachu.
Mikate hiyo itakatwakatwa na kumiminiwa mafuta. Hiyo ni sadaka ya ngano.
Sadaka hiyo ikipikiwa katika vyombo vya udongo, vyombo hivyo vitavunjwa. Lakini ikiwa vyombo hivyo ni vya shaba, basi, vitasafishwa vizuri kwa maji.
Ikiwa mutu anatoa sadaka hiyo kwa kumushukuru Mungu, basi, ataitoa pamoja na maandazi yasiyotiwa chachu yaliyopakwa mafuta, mikate myembamba iliyopakwa mafuta na maandazi ya unga laini uliochanganywa na mafuta.
Sadaka yoyote ya ngano iliyopikwa juu ya mafika katika chungu au katika kikaango itakuwa mali ya kuhani anayeitolea.