Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Walawi 2:3 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

3 Sehemu inayobaki ya sadaka hiyo ni ya makuhani. Hiyo ni sehemu takatifu kabisa ya sadaka Yawe anayotolewa kwa moto.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Walawi 2:3
17 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Mutawala akawaambia kwamba hawaruhusiwi kushiriki chakula kitakatifu sana, mpaka kukuwe kuhani atakayeweza kutoa shauri kwa njia Urimu na Tumimu.


Kwa siku saba utafanyia mazabahu upatanisho na kuitakasa. Nyuma ya hayo, mazabahu itakuwa takatifu kabisa na chochote kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu.


Watakula sadaka ya vyakula, sadaka ya kusamehewa zambi, na sadaka ya malipo ya kosa. Kila kitu katika Israeli kilichotakaswa kwa Mungu kitakuwa chao.


akaniambia hivi: Hapa ndipo makuhani watakapopikia nyama ya sadaka ya malipo ya kosa, sadaka ya kusamehewa zambi, na kupika sadaka za vyakula. Kwa hiyo hawatoki inje ya baraza na chochote, kusudi watu wasijichafue kwa kugusa kitu kitakatifu.


Ule muguu uliotolewa na kilali cha sadaka ya kufanyia kitambulisho cha kumutolea Yawe watavileta pamoja na sadaka za mafuta zinazotolewa kwa moto, kwa kufanya kitambulisho cha kuvitolea mbele ya Yawe, vikuwe sadaka ya kutolewa kwa kitambulisho. Hivyo vitakuwa vyako pamoja na wana wako; ni haki yenu milele kama vile Yawe alivyoamuru.


Kisha atachinja yule mwana-kondoo katika Pahali Patakatifu, wanapochinjia nyama wa sadaka kwa ajili ya zambi na sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Sadaka hii kwa ajili ya kosa na vilevile sadaka kwa ajili ya zambi, ni mali ya kuhani. Ni sadaka takatifu kabisa.


Sehemu inayobaki ya sadaka ya ngano, ni ya makuhani. Hiyo ni sehemu takatifu kabisa ya sadaka inayotolewa Yawe kwa moto.


Mutu huyo anaweza kula mukate wa Mungu wake, vitu vitakatifu na vile vitakatifu kabisa.


Basi, kuhani atamufanyia yule mutu ibada ya upatanisho kwa ajili ya zambi, naye atasamehewa. Unga unaobaki utakuwa wa kuhani kama vile inavyofanyika juu ya sadaka ya ngano.


Unga uliobakia Haruni na wazao wake makuhani wataukula bila kutiwa chachu. Wataukula kwenye Pahali Patakatifu katika kiwanja cha hema la mukutano.


Sheria ni moja kuelekea sadaka kwa ajili ya kosa na sadaka kwa ajili ya zambi. Kuhani anayefanya ibada ya upatanisho ndiye atakayeitwaa.


Sadaka yoyote ya ngano iliyopikwa juu ya mafika katika chungu au katika kikaango itakuwa mali ya kuhani anayeitolea.


Kati ya vitu vitakatifu kabisa ambavyo haviteketezwi kwa moto, hivi vitakuwa vyenu: sadaka za vyakula, sadaka kwa ajili ya zambi na sadaka za kosa. Kila kitu watu watakachonitolea kama vile sadaka takatifu kitakuwa chako na wana wako.


Kati ya makabila yote ya Israeli nilimuchagua Haruni na jamaa yake kuwa makuhani wangu, wanitumikie kwenye mazabahu, wafukize ubani na kuvaa kizibao mbele yangu. Nikaipatia jamaa ya babu yako sadaka zangu ambazo Waisraeli walinitolea kwa moto.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ