mikate isiyotiwa chachu, maandazi yasiyotiwa chachu yaliyopondwa kwa mafuta, na mikate myembamba isiyotiwa chachu, lakini iliyopakwa mafuta. Vyote hivi vikuwe vimetengenezwa kwa unga laini wa ngano.
Ukimutolea Yawe sadaka ya mazao yako ya kwanza utaitoa hiyo ikiwa imechomwa katika masuke yake, au utaitoa katika mikate ya kuchomwa iliyotengenezwa kwa ngano iliyosagwa.
Kuhani atateketeza sehemu ya sadaka hiyo ya ngano iliyopondwa na mafuta pamoja na ubani wake wote, ikuwe sadaka ya ukumbusho. Hiyo ni sadaka Yawe anayotolewa kwa moto.
Ikiwa hawezi kutoa hua wawili au vitoto viwili vya njiwa kama vile sadaka yake kwa ajili ya zambi aliyotenda, basi, ataleta unga kilo moja. Lakini hatautia mafuta wala ubani maana ni sadaka kwa ajili ya zambi.
basi, yule anayetoa sadaka yake, atamuletea vilevile Yawe sadaka ya vyakula ya kilo moja ya unga laini uliopondwa na kuchanganywa na litre moja ya mafuta.