Kore mwana wa Imuna, Mulawi, aliyekuwa mulinzi wa Mulango wa Mashariki wa hekalu, akasimamia matoleo yote ya mapenzi kwa Mungu; na kugawanya matoleo kwa ajili ya Yawe na sadaka zinazokuwa takatifu kabisa.
akaniambia hivi: Hapa ndipo makuhani watakapopikia nyama ya sadaka ya malipo ya kosa, sadaka ya kusamehewa zambi, na kupika sadaka za vyakula. Kwa hiyo hawatoki inje ya baraza na chochote, kusudi watu wasijichafue kwa kugusa kitu kitakatifu.
Musa akamwambia Haruni na wana wake waliobakia, Eleazari na Itamari: Mutwae ile sehemu ya sadaka ya vyakula iliyobakia kutoka sadaka Yawe anazotolewa kwa moto. Muikule karibu na mazabahu bila kutiwa chachu kwa sababu ni takatifu kabisa.
Kisha atachinja yule mwana-kondoo katika Pahali Patakatifu, wanapochinjia nyama wa sadaka kwa ajili ya zambi na sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Sadaka hii kwa ajili ya kosa na vilevile sadaka kwa ajili ya zambi, ni mali ya kuhani. Ni sadaka takatifu kabisa.
Basi, kuhani atamufanyia yule mutu ibada ya upatanisho kwa ajili ya zambi, naye atasamehewa. Unga unaobaki utakuwa wa kuhani kama vile inavyofanyika juu ya sadaka ya ngano.
Lakini kama damu ya sadaka yoyote kwa ajili ya zambi imeletwa ndani ya hema la mukutano kwa kufanya ibada ya upatanisho katika Pahali Patakatifu, sadaka hiyo itateketezwa kwa moto.
Kati ya vitu vitakatifu kabisa ambavyo haviteketezwi kwa moto, hivi vitakuwa vyenu: sadaka za vyakula, sadaka kwa ajili ya zambi na sadaka za kosa. Kila kitu watu watakachonitolea kama vile sadaka takatifu kitakuwa chako na wana wako.
Kati ya makabila yote ya Israeli nilimuchagua Haruni na jamaa yake kuwa makuhani wangu, wanitumikie kwenye mazabahu, wafukize ubani na kuvaa kizibao mbele yangu. Nikaipatia jamaa ya babu yako sadaka zangu ambazo Waisraeli walinitolea kwa moto.