Musirudie kukusanya kila kitu katika shamba la mizabibu, wala usiokote zabibu zilizoanguka chini. Utawaachia wamasikini na wageni. Mimi ni Yawe, Mungu wenu.
Unapovuna mavuno yako katika shamba, usivune kabisa mpaka kwenye mupaka wa shamba lako wala usirudi nyuma kukusanya mabaki. Utawaachia hayo wamasikini na wageni. Mimi ni Yawe, Mungu wenu.
Siku moja, Ruta wa Moabu akamwambia Naomi: “Muniruhusu niende kukusanya masalio ya mavuno pahali nitakapopata kukubaliwa na mwenye shamba.” Naomi akamwambia: “Basi, uende binti yangu.”
Halafu Boazi akamwambia Ruta: “Sasa sikiliza binti yangu. Usiende kuokota masuke pahali pengine, lakini katika shamba hili tu. Ushikamane na wanawake hawa.