Usiku ule wakamulewesha baba yao kwa divai. Yule binti wa kwanza akakwenda akalala naye. Lakini baba yake hakujua wakati binti yake alipolala naye, wala wakati alipoondoka.
Lakini inafaa tuwaandikie kwa kuwaambia kwamba wajitenge na vitu vilivyochafuliwa kwa kutambikia sanamu, waepuke uasherati na wasikule nyamafu wala damu.