Lakini yule beberu aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Azazeli atatolewa mbele ya Yawe akiwa muzima. Kwa kufanya ibada ya upatanisho, kuhani atamwacha aende katika jangwa kwa Azazeli, kwa ajili ya zambi za jamii.
Kisha wale watumishi wa mashua wakasemezana: Tupige kura tupate kujua hasara hii imetupata kwa ajili ya kosa la nani. Basi, wakapiga kura; kura ikamwangukia Yona.