Kwa maana, tunajua kwamba hema hii tunayoishi ndani yake hapa katika dunia, maana yake mwili wetu, itakapobomolewa, Mungu atatupatia makao mengine mbinguni. Nayo ni nyumba aliyoijenga yeye mwenyewe na inayodumu milele.
Yeye atabadilisha huu mwili wetu wa uzaifu na kuufananisha na mwili wake wa utukufu kwa nguvu ambayo kwa njia yake anaweza kuwa na mamlaka juu ya vitu vyote.