Kwa pahali pa harufu ya marasi watatoa uvundo; kwa pahali pa mikaba mizuri watatumia kamba; kwa pahali pa nywele nzuri watakuwa na upaa; kwa pahali pa nguo nzuri watavaa magunia; uzuri wao wote utageuka kuwa haya.
kuhani atapaangalia. Kama akiona kwamba nywele zimegeuka kuwa nyeupe na pana shimo, basi, huo ni ukoma. Ukoma huo umejitokeza kwa njia ya pahali pale palipoungua. Kuhani atamutangaza mutu yule kuwa muchafu, maana ana ugonjwa wa ukoma.