Utwae pamoja nawe nyama wote wanaohesabiwa kuwa safi, dume saba na dike saba ya kila aina. Lakini nyama wanaohesabiwa kuwa wachafu, utwae dume na dike ya kila aina.
Lakini chochote kinachoishi katika bahari au ndani ya mito, ambacho hakina mapezi wala magamba, maana viumbe vyote vinavyotembea ndani ya maji na viumbe vingine vyote vinavyoishi ndani ya maji ni vichafu kwenu.
Au kama mutu yeyote kati yenu akijichafua bila kukusudia kwa kugusa kitu chochote kichafu, ikuwe ni muzoga wa nyama wa pori au wa kufugwa au wadudu, atakuwa na kosa.