Walawi 10:14 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 200214 Lakini kilali ambacho wanafanya nacho kitambulisho cha kumutolea Yawe na muguu unaotolewa sadaka kama vile kitambulisho, munaweza kuvikulia pahali popote pasipo kuwa pachafu. Utakula wewe na watoto wako wanaume na wanawake. Vitu hivyo umepewa kama haki yako na ya wazao wako kutoka sadaka za amani za watu wa Israeli. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Yule mutu akaniambia: Vyumba hivi vyote ni vitakatifu. Ndani ya vyumba hivi makuhani wanaoingia mbele ya Yawe, wanakula sadaka takatifu kabisa: sadaka takatifu kabisa na humo ndimo munamowekwa sadaka za vyakula, sadaka za kuomba kusamehewa zambi na sadaka kwa ajili ya malipo ya kosa kwa sababu pahali hapo ni patakatifu.