Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Walawi 10:13 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

13 Mutaikula katika Pahali Patakatifu kwa sababu hiyo ni haki yako na wazao wako kutoka katika sadaka Yawe anazotolewa kwa moto. Hivi ndivyo nilivyoamuriwa.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Walawi 10:13
7 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Yule mutu akaniambia: Vyumba hivi vyote ni vitakatifu. Ndani ya vyumba hivi makuhani wanaoingia mbele ya Yawe, wanakula sadaka takatifu kabisa: sadaka takatifu kabisa na humo ndimo munamowekwa sadaka za vyakula, sadaka za kuomba kusamehewa zambi na sadaka kwa ajili ya malipo ya kosa kwa sababu pahali hapo ni patakatifu.


Musa akamwambia Haruni na wana wake waliobakia, Eleazari na Itamari: Mutwae ile sehemu ya sadaka ya vyakula iliyobakia kutoka sadaka Yawe anazotolewa kwa moto. Muikule karibu na mazabahu bila kutiwa chachu kwa sababu ni takatifu kabisa.


Lakini kilali ambacho wanafanya nacho kitambulisho cha kumutolea Yawe na muguu unaotolewa sadaka kama vile kitambulisho, munaweza kuvikulia pahali popote pasipo kuwa pachafu. Utakula wewe na watoto wako wanaume na wanawake. Vitu hivyo umepewa kama haki yako na ya wazao wako kutoka sadaka za amani za watu wa Israeli.


Sehemu inayobaki ya sadaka hiyo ni ya makuhani. Hiyo ni sehemu takatifu kabisa ya sadaka Yawe anayotolewa kwa moto.


Sadaka yoyote ya ngano iliyotolewa na kuhani itateketezwa yote; haitakuliwa hata kidogo.


Mutavikula vitu hivyo kama vitu vitakatifu kabisa, na ni wanaume tu ndio watakaovikula; vitu hivyo ni vitakatifu kwenu.


Na kila kitu kitakatifu cha mutu kitakuwa cha kuhani; kitu chochote mutu anachomutolea kuhani kitakuwa chake.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ