Walawi 1:9 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20029 Lakini matumbotumbo na miguu ya nyama yule vitasafishwa kwa maji. Kuhani atateketeza sadaka yote juu ya mazabahu. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumupendeza Yawe. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Haruni na wazao wake ndio waliokuwa wakitoa sadaka juu ya mazabahu ya sadaka za kuteketezwa kwa moto na vilevile juu ya mazabahu ya kufukizia ubani. Walifanya kazi zote zilizoelekea Pahali Patakatifu Sana kwa kuifanyia Israeli upatanisho. Haya yote waliyafanya kulingana na maagizo Musa, mutumishi wa Mungu aliyotoa.