Walitoa vilevile sadaka za kawaida ambazo ziliteketezwa nzima, sadaka zilizotolewa wakati wa sikukuu ya mwandamo wa mwezi na katika sikukuu nyingine zote alizoagiza Yawe. Vilevile walitoa sadaka zote za mapenzi.
Ninyi mutanijengea mazabahu ya udongo. Juu yake mutanitolea kondoo wenu na ngombe wenu kama sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani. Pahali popote nitakapowakumbusha watu jina langu, pale pale mimi mwenyewe nitawafikia na kuwabariki.
mukinitolea mimi Yawe sadaka kutoka katika mifugo yenu, sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya kutimiza kiapo au kutoa sadaka ya mapenzi au sadaka ya wakati wa sikukuu zenu zilizowekwa, na kufanya harufu nzuri ya kunipendeza mimi Yawe,
basi wote wawili watakwenda kwa kuhani na kupeleka sadaka inayotakiwa, ni kusema sehemu ya kumi ya unga wa shayiri; lakini bila kuitia mafuta au ubani, kwa sababu ni sadaka ya vyakula ya mume anayekuwa na wivu kwa muke wake, kwa ukumbusho wa kosa.
Lakini ninyi munasema kwamba mutu akiwa na kitu cha kumusaidia baba au mama yake, lakini akimwambia kwamba kitu kile ni Korbane, (maana yake, kimetolewa kuwa sadaka takatifu kwa Mungu),
Basi wandugu zangu, kufuatana na vile Mungu alivyoonyesha huruma yake kwetu, ninawasihi mujitoe wenyewe kwake kuwa sadaka yenye uzima, takatifu na yenye kumupendeza. Hii ndiyo njia ya kweli ya kumwabudu.
Muishi katika upendo kama vile Kristo alivyotupenda na kutoa maisha yake kwa ajili yetu kama vile matoleo na sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri inayomupendeza Mungu.