Bwana wetu Yawe akaniambia. Wewe mwanadamu! Yawe anasema hivi: Wakati mazabahu itakapojengwa utaitakasa, kwa kutoa sadaka za kuteketezwa juu yake na kuinyunyizia damu ya nyama waliotolewa.
Kisha Mungu akaniambia: Wewe mwanadamu, angalia upande wa kaskazini. Nami nikaangalia upande wa kaskazini, na huko upande wa kaskazini wa mulango wa mazabahu, niliona ile sanamu iliyomuchukiza Mungu.
Kisha, atamuchinja huyo ngombe mbele ya Yawe. Nao makuhani wazao wa Haruni wataichukua damu na kuinyunyizia mazabahu inayokuwa kwenye mulango wa hema la mukutano, pande zake zote.
Kisha atachinja yule mwana-kondoo katika Pahali Patakatifu, wanapochinjia nyama wa sadaka kwa ajili ya zambi na sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Sadaka hii kwa ajili ya kosa na vilevile sadaka kwa ajili ya zambi, ni mali ya kuhani. Ni sadaka takatifu kabisa.
Nyama wa sadaka kwa ajili ya kosa atachinjiwa pahali wanapochinjiwa nyama wa sadaka za kuteketezwa kwa moto na damu yake itanyunyizwa juu ya mazabahu pande zake zote.