Wafilipi 3:21 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
21 Yeye atabadilisha huu mwili wetu wa uzaifu na kuufananisha na mwili wake wa utukufu kwa nguvu ambayo kwa njia yake anaweza kuwa na mamlaka juu ya vitu vyote.
Bwana wetu Yawe atakiangamiza kifo milele! Atayafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuondoa haya ya watu wake katika dunia yote. Yawe amesema hivyo.
Wafu wako wataishi tena, miili yao itafufuka. Wanaolala katika mavumbi wataamuka na kuimba kwa furaha! Mungu atapeleka umande wake wa uzima, nao wanaokuwa kwa wafu watatoka wazima.
Inanipasa kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifo! Ewe kifo, mapigo yako ni wapi? Ewe kuzimu, kuangamiza kwako ni wapi? Mimi sitawaonea tena huruma!
Kwa maana wale Mungu aliowachagua tangu zamani, ndio aliofanya mupango juu yao tangu zamani, apate kuwafananisha na Mwana wake, kusudi Mwana wake akuwe muzaliwa wa kwanza wa wandugu wengi.
Wapendwa wangu, sasa sisi ni watoto wa Mungu, wala namna tutakavyokuwa haijaonekana bado waziwazi. Lakini tunajua kwamba wakati Kristo atakapotokea, tutafanana naye kwa sababu tutamwona vile anavyokuwa.