Kwa hiyo, Abramu akaondoka kama vile Yawe alivyomwamuru, na Loti akakwenda pamoja naye. Abramu alikuwa na umri wa miaka makumi saba na mitano alipotoka Harani.
Kwa sababu hii, Kristo ni mupatanishi wa agano jipya. Kwa njia ya kufa kwake aliwakomboa watu toka katika makosa waliyofanya chini ya uongozi wa agano la kwanza, kusudi wale walioalikwa na Mungu wapate kupokea urizi wa milele aliowaahidia.