Mimi Yawe nimesema: Hakika nitawatendea hivyo ninyi wote muliokusanyika hapa kwa kunipinga. Wote wataishia humuhumu katika jangwa na ni humu watakamokufia.
Miaka makumi tatu na nane ilikuwa imepita tangu kuondoka Kadesi-Barnea mpaka kuvuka kijito Zeredi. Wakati huo, wote wenye umri wa kwenda kwa vita waliotoka Misri walikuwa wamekwisha kufa, kulingana na jinsi Yawe alivyowaapia.
Lakini sasa sisi tulioamini, tutaingia kwenye mapumziko ambayo Mungu alitaja aliposema: “Halafu nikaapa kwa kasirani kwamba hawataingia hata kidogo kwenye mapumziko niliyowatayarishia!” Mungu alisema vile ingawa alikuwa amemaliza kazi zake tangu pale alipoumba dunia.