Majaribu yale munayopata, ni yale yanayowapata watu wengine wote. Mungu hatawaachilia kujaribiwa kupita nguvu zenu, kwa maana yeye ni mwaminifu. Jaribu litakapowatokea, atawapatia nguvu ya kulivumilia, hata muweze kulishinda.
Yeye atabadilisha huu mwili wetu wa uzaifu na kuufananisha na mwili wake wa utukufu kwa nguvu ambayo kwa njia yake anaweza kuwa na mamlaka juu ya vitu vyote.
na kwa sababu hiyo ninapata mateso haya. Lakini sisikii haya kwa ajili ya ile. Maana ninajua ni nani yule niliyemwamini, nami ninahakikisha kwamba anaweza kuchunga kile alichonipa kwa kunilinda mpaka Siku ile ya kurudi kwake.
Kufuatana na vile ulivyojichunga katika uvumilivu sawa nilivyokuagiza, mimi vilevile nitakuchunga na hasara wakati itakapokuja katika dunia yote kwa kuwajaribu wakaaji wake.