19 Ninawasihi sana kuomba Mungu, kusudi nipate kurudishwa kwenu upesi.
Lakini pamoja na maneno haya, unitayarishie vilevile pahali pa kukaa, maana ninatumaini kwamba Mungu atajibu maombi yenu, na kunijalia nipate kurudishwa tena kwenu.
Wandugu, ninawasihi kupokea kwa uvumilivu haya maonyo ninayowatolea kwa maana nimewaandikia kwa kifupi.