Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Waebrania 13:11 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

11 Kuhani Mukubwa anapeleka damu ya nyama ndani ya Pahali Patakatifu Sana kwa ajili ya kuitoa kuwa sadaka ya kusamehewa zambi lakini viungo vyote vya nyama wale vinateketezwa kwa moto mbali na kambi.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Waebrania 13:11
13 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Lakini nyama ya ngombe dume yule pamoja na ngozi na mavi yake utavitwaa na kuviteketeza inje ya kambi yenu. Hii itakuwa sadaka ya kuondoa zambi.


Utatwaa vilevile ngombe dume aliyetolewa kuwa sadaka ya kusamehewa zambi; watamuteketeza katika pahali palipochaguliwa ndani ya nyumba ya Yawe, lakini inje ya Pahali Patakatifu.


Yule ngombe dume na mbuzi waliotolewa sadaka kwa ajili ya zambi ambao damu yao ilipelekwa katika Pahali Patakatifu kwa kufanya ibada ya upatanisho, watapelekwa inje ya kambi na kuteketezwa kwa moto. Ngozi zao, nyama na mavi yao, vyote vitateketezwa kwa moto.


Wazao wanaume wa Haruni ndio peke yao wanaoruhusiwa kula sehemu hiyo maana hiyo imetengwa siku zote kwa ajili yao kutoka sadaka Yawe anazotolewa kwa moto. Yeyote atakayezigusa atakuwa mutakatifu.


Lakini nyama na ngozi akaviteketeza kwa moto inje ya kambi.


Wana wake wakamuletea damu, naye akachovya kidole chake katika damu hiyo na kuipakaa kwenye pembe za mazabahu. Damu iliyobakia akaimwanga kwenye tako la mazabahu.


Ninyi mutamupa kuhani Eleazari ngombe huyo. Atatolewa inje ya kambi na kuchinjwa mbele ya kuhani huyo.


Nyuma ya hayo, kuhani atafua nguo zake na kuoga mwili kwa maji, halafu anaweza kuingia katika kambi; atakuwa muchafu mpaka magaribi.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ