Waamuzi 7:5 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
5 Basi, Gideoni akawapeleka watu kwenye muto na Yawe akamwambia: “Watu watakaolamba maji kwa ulimi kama imbwa, utawatenganisha na wale watakaopiga magoti kwa kunywa maji.”
Elia akamwambia: “Usiogope. Kwenda ufanye kama vile ulivyosema. Lakini unitengenezee mimi kwanza na kuniletea andazi dogo, kisha ujitengenezee wewe na mwana wako chakula.
Jumla ya waliokunywa maji kwa kuchota kwa mikono yao na kulamba kama imbwa ilikuwa mia tatu. Lakini wengine wote waliobaki walipiga magoti kwa kunywa maji.