Halafu wakalundika mawe mengi juu yake, ambayo yako mpaka leo. Hapo hasira ya Yawe ikapoa; na pahali pale pakaitwa Bonde la Akori, ni kusema Bonde la Taabu, mpaka hivi leo.
Malaika wa Yawe aliondoka Gilgali, akaenda Bokimu, akawaambia Waisraeli: “Niliwaondoa katika inchi ya Misri na kuwaleta katika inchi ambayo niliahidi kwa kiapo kwa babu zenu. Nilisema kwamba sitalivunja agano langu nanyi hata kidogo.
Kwa hiyo Samweli alitwaa mwana-kondoo anayenyonya akamutolea Yawe kama sadaka ya kuteketezwa. Kisha Samweli akamulilia Yawe kwa ajili ya Waisraeli, naye akajibu kilio chake.