Alipofika Lehi, Wafilistini wakamwendea mbio na walikuwa wanapiga kelele. Kwa rafla roho wa Yawe akamushika Samusoni kwa nguvu na zile kamba walizomufunga kwenye mikono yake zikakatika kama kitani kilichoguswa na moto, navyo vifungo vikaanguka chini.
Mungu akafungua pahali palipokuwa shimo kule Lehi, akatiririsha maji. Samusoni akakunywa maji hayo na nguvu zake zikamurudilia. Chemichemi hiyo ikaitwa “Kisima cha Yule Anayeita” nayo iko kule Lehi mpaka leo.