Waamuzi 1:4 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
4 Basi watu wa kabila la Yuda wakaenda kufanya mashambulio, naye Yawe akawatia Wakanana na Waperizi katika mikono yao, wakawaua watu elfu kumi katika vita kule Bezeki.
Mujue leo hii kwamba anayewatangulia kama vile moto unaoteketeza miti ni Yawe, Mungu wenu. Atawaangamiza na kuwashinda mbele yenu, kwa hiyo mutawafukuza na kuwaangamiza mara moja, kama vile Yawe alivyowaahidi.
Watu wa kabila la Yuda wakawaambia wandugu zao, watu wa kabila la Simeoni: “Mushirikiane nasi tunapokwenda kuitwaa inchi hiyo ambayo tumepewa. Nasi, vilevile tutashirikiana nanyi kwenda kuitwaa inchi mutakayopewa.” Hivyo kabila la Simeoni likakubali kushirikiana nao.
Yonatani akamwambia yule kijana aliyemubebea silaha: “Kuja, tuende kwenye ile kambi ya hawa watu wasiotahiriwa. Labda Yawe atatusaidia, maana Yawe haokoi kwa kutegemea wingi au uchache wa watu.”