Ufunuo 15:2 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20022 Tena nikaona kitu kinachofanana na bahari ya kioo, iliyochanganyika na moto. Nikaona vilevile wale walioshinda yule nyama wa ajabu pamoja na sanamu yake na tarakimu zinazolingana na herufi za jina lake. Watu wale walikuwa wakisimama juu ya ile bahari ya kioo wakishika vinubi walivyopewa na Mungu. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Majaribu hayo ni kwa ajili ya kupima imani yenu. Zahabu ni kitu kinachoharibika, lakini ingawa vile inapimwa kwa njia ya kuchomwa ndani ya moto. Hivi vilevile imani yenu inayokuwa ya bei kali kuliko zahabu, inapaswa kupimwa kusudi ijulikane kuwa ya kweli. Na kwa sababu hii mutapata sifa, utukufu na heshima wakati Yesu Kristo atakapotokea.