Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Ufunuo 11:7 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

7 Wakati watakapomaliza kutoa huo ushuhuda wa Mungu, yule nyama wa ajabu anayetoka katika kuzimu atapigana vita nao, naye atawashinda na kuwaua.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Ufunuo 11:7
20 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Huyo atasema maneno ya kujivuna mbele ya Mungu Mukubwa na kuwatesa watakatifu wake. Atajaribu kubadilisha sikukuu na sheria zao, na watakatifu watatiwa katika mikono yake kwa muda wa miaka mitatu na nusu.


Yesu akawajibu: “Mwende kumwambia yule mbweha: ‘Leo na kesho nitafukuza pepo na kuponyesha wagonjwa, na kesho kutwa nitamaliza kazi yangu.’


Nao wale pepo walimusihi Yesu kwamba atakapowafukuza asiwaamuru kutumbukia ndani ya shimo lisilokuwa na mwisho.


Mimi nimekutukuza wewe katika dunia kwa kuwa nimemaliza kazi ile uliyonipa.


Wakati Yesu alipokwisha kumeza ile divai, akasema: “Yote yametimilika!” Kisha akainamisha kichwa na kukata roho.


Lakini sihesabu maisha yangu kuwa kitu cha bei kali kwangu. Shabaha moja ninayokuwa nayo ni kufikia mwisho wa utumishi wangu na kutimiza kazi ile niliyopewa na Bwana Yesu; maana yake kushuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu.


Nimeshindana vizuri, nimekimbia na kufika mwisho wa mashindano yangu. Nimelinda imani yangu.


Nami nitawatuma washuhuda wangu wawili, wakiwa wamevaa nguo za kilio. Nao watatangaza ujumbe wa Mungu kwa muda wa siku elfu moja mia mbili na makumi sita.”


Yule nyoka akamukasirikia yule mwanamuke na kwenda kufanya vita na wazao wake wengine; ndio wale wanaoshika amri za Mungu na kufuata ukweli ulioshuhudiwa na Yesu Kristo.


Kisha nikaona nyama wa pili wa ajabu akitokea ndani ya udongo. Alikuwa na pembe mbili zinazokuwa kama za mwana-kondoo naye alikuwa akisema kama nyoka mukubwa.


Akapewa ruhusa ya kupigana vita na watu wa Mungu na kuwashinda. Akapewa hata mamlaka ya kutawala watu wote, wa kila kabila, kila jamaa, kila luga na kila taifa.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ