Ufunuo 11:3 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20023 Nami nitawatuma washuhuda wangu wawili, wakiwa wamevaa nguo za kilio. Nao watatangaza ujumbe wa Mungu kwa muda wa siku elfu moja mia mbili na makumi sita.” အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Yule mutu aliyesimama upande wa juu wa muto, aliyevaa nguo za kitani, akainua mikono yake yote miwili kuelekea mbinguni. Kisha nikamusikia akiapa kwa jina la yule anayeishi milele: Itakuwa muda wa nyakati tatu na nusu. Wakati mateso ya watu watakatifu yatakapokomeshwa, mambo haya yote yatakuwa yametimia.
Kisha nikaona viti vya kifalme na watu waliokuwa wakiikaa juu yao, wakapewa uwezo wa kuhukumu. Nikaona vilevile roho za wale waliochinjwa kwa sababu ya kutangaza ukweli ulioshuhudiwa na Yesu na Neno la Mungu. Watu wale hawakumwabudu yule nyama wa ajabu, wala sanamu yake, wala hawakupigwa chapa yake juu ya paji za nyuso zao, au juu ya mikono yao. Nao wakafufuka na kutawala pamoja na Kristo muda wa miaka elfu moja.