Ufunuo 1:9 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20029 Mimi ni ndugu yenu Yoane. Kwa njia ya kuungana na Yesu, ninashirikiana nanyi katika mateso, katika ufalme wake na katika kuvumilia. Mimi nilikuwa nimepelekwa katika kisanga kinachoitwa Patimo, kwa sababu nilihubiri Neno la Mungu na ukweli ulioshuhudiwa na Yesu. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Kisha nikaona viti vya kifalme na watu waliokuwa wakiikaa juu yao, wakapewa uwezo wa kuhukumu. Nikaona vilevile roho za wale waliochinjwa kwa sababu ya kutangaza ukweli ulioshuhudiwa na Yesu na Neno la Mungu. Watu wale hawakumwabudu yule nyama wa ajabu, wala sanamu yake, wala hawakupigwa chapa yake juu ya paji za nyuso zao, au juu ya mikono yao. Nao wakafufuka na kutawala pamoja na Kristo muda wa miaka elfu moja.