Ufunuo 1:2 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20022 Naye Yoane alishuhudia kwamba mambo yote aliyoona yanaelekea Neno la Mungu na ukweli ulioshuhudiwa na Yesu Kristo. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Kisha nikaona viti vya kifalme na watu waliokuwa wakiikaa juu yao, wakapewa uwezo wa kuhukumu. Nikaona vilevile roho za wale waliochinjwa kwa sababu ya kutangaza ukweli ulioshuhudiwa na Yesu na Neno la Mungu. Watu wale hawakumwabudu yule nyama wa ajabu, wala sanamu yake, wala hawakupigwa chapa yake juu ya paji za nyuso zao, au juu ya mikono yao. Nao wakafufuka na kutawala pamoja na Kristo muda wa miaka elfu moja.