Mimi Paulo ninawatumia salamu zangu, nikiziandika kwa mukono wangu mwenyewe. Musisahau kwamba mimi ningali katika kifungo. Ninawatakia neema kutoka kwa Mungu.
Ninakuandikia wewe Timoteo mwana wangu wa kweli katika imani. Ninakutakia neema na rehema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.