Haukutuacha tuishi katika utumwa ingawa tulikuwa watumwa. Uliwafanya wafalme wa Persia wakuwe wema kwetu na kuturuhusu tuishi na kuijenga nyumba yako iliyokuwa imebomoka, na ukatufanya tukae salama hapa Yuda na Yerusalema.
Kwa hiyo mutawatumikia waadui zenu ambao Yawe atawatuma mbele yenu, kwa njaa, kiu na uchi, na ukosefu wa kila kitu. Atawafunga nira ya chuma mpaka awaangamize.