Sizani kama utafanya hivyo, kuwaua watu wa haki pamoja na waovu, kutendea watu wa haki sawa na waovu. Hapana, haiwezekani! Mwamuzi wa dunia yote hataacha kutenda mambo yanayokuwa sawa!”
Ee Yawe, Mungu wa Israeli, wewe ni mwenye haki na umetuacha tubaki kama vile tunavyokuwa hivi leo. Tunaungama makosa yetu mbele yako, tukijua kwamba hakuna anayekuwa na haki yoyote ya kuja mbele yako kwa ajili ya makosa haya.”
Ukamwona kuwa wa haki mbele yako; ukafanya agano naye kuwapa wazao wake inchi ya Wakanana, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wayebusi na Wagirgasi. Na ahadi yako ukaitimiza; maana wewe ni mwaminifu.
Ee Yawe, wewe ni mwenye haki, ingawa nitakushitaki. Lakini ningependa nibishane nawe juu ya mambo ya haki: Kwa nini waovu wanafanikiwa katika mambo yao? Mbona wote wanaodanganya wanastawi?
Imekuwa hivyo kwa sababu ya uovu walioufanya, wakanikasirikisha kwa kuifukizia ubani na kuitumikia miungu mingine ambayo wao wenyewe hawakuifahamu, wala ninyi, wala babu zenu.
Lakini Yawe amefanya sawa kwa maana nimeliasi neno lake. Munisikilize enyi watu wote, muyaangalie mateso yangu. Wabinti zangu na vijana wangu wanaume wamepelekwa katika utumwa.
Nanyi mutatambua kwamba mimi ni Yawe ambaye hamukufuata masharti yake na maagizo yake hamukuyatimiza, lakini mumetenda kufuatana na maagizo ya mataifa yanayowazunguka.