Nehemia 8:14 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
14 Wakagundua kwamba, imeandikwa katika kitabu cha Sheria kuwa Yawe alimwamuru Musa, kwamba watu wanapaswa kukaa katika vibanda wakati wa sikukuu ya mwezi wa saba.
Lakini Yakobo akasafiri kwenda Sukoti, na kule akajijengea nyumba na vibanda kwa ajili ya nyama wake. Kwa sababu hiyo, pahali hapo pakaitwa Sukoti, ni kusema “Vibanda”.