Kuhani, wa uzao wa Haruni atakuwa pamoja na Walawi wanapokea zaka. Halafu Walawi watapeleka sehemu moja ya kumi ya zaka zote zilizotolewa katika nyumba ya Mungu kwenye vyumba na gala.
Nikawakaripia na kuwalaani, hata nikawapiga wamoja kati yao na kuwaongoa nywele zao. Nikawalazimisha kuapa kwa jina la Mungu, nikisema: “Wabinti zenu musiwaoeshe kwa vijana wao, wala wabinti zao wasiolewe na vijana wenu au na ninyi wenyewe.