Yuda na wana wake: Eri, Onani, Sela, Peresi na Zera. (Lakini Eri na Onani walikufa katika inchi ya Kanana). Wana wa Peresi walikuwa Hesironi na Hamuli.
Kazi yao ilikuwa ni kuwasaidia makuhani wa ukoo wa Haruni katika kazi ya kujenga nyumba ya Yawe, kutunza viwanja na vyumba, kusafisha vyombo vitakatifu vyote na kufanya kazi zinazoelekea kujenga nyumba ya Yawe.
Sehemu inayofuata ikajengwa upya na Meremoti mwana wa Uria, mujukuu wa Hakosi. Sehemu inayofuata ikajengwa upya na Mesulamu mwana wa Berekia, mujukuu wa Mesezabeli. Sehemu inayofuata ikajengwa upya na Zadoki mwana wa Bana.