Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Nehemia 10:34 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

34 kwa ajili ya mikate mitakatifu, sadaka za unga za kawaida, sadaka za kuteketezwa kwa moto za kawaida, sadaka za siku za Sabato, sikukuu za mwandamo wa mwezi, sikukuu nyingine zilizowekwa, vitu vingine vitakatifu, sadaka za kusamehewa zambi, kwa kuwafanyia upatanisho watu wa Israeli na kazi nyingine zozote za nyumba ya Mungu wetu.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Nehemia 10:34
16 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Waligawanywa kwa kupiga kura maana kulikuwa wakubwa wa Pahali Patakatifu na viongozi wa Mungu kati ya ukoo zote mbili; ukoo wa Eleazari na ukoo wa Itamari.


Kura ya kwanza ikamwangukia Yoyaribu, ya pili Yedaya, ya tatu Harimu, ya ine Seorimu, ya tano Malkia, ya sita Miyamini, ya saba Hakosi, ya nane Abiya, ya kenda Yesua, ya kumi Sekania, ya kumi na moja Eliasibu, ya kumi na mbili Yakimu, ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na ine Yesebeabu, ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri, ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi, ya kumi na kenda Petahia, ya makumi mbili Yehezekeli, ya makumi mbili na moja Yakini, ya makumi mbili na mbili Gamuli, ya makumi mbili na tatu Delaya, ya makumi mbili na ine Mazia.


Ninataka kujenga nyumba ya kumwabudia Yawe wangu. Nitaitakasa kwa ajili yake, nayo itakuwa pahali pa kufukiza ubani wenye harufu nzuri mbele yake, na vilevile pahali pa kumutolea mikate mitakatifu siku zote, na sadaka za kuteketezwa asubui na magaribi na za siku za Sabato, za Mwandamo wa Mwezi, na sikukuu zingine za Yawe, Mungu wetu, kama vile alivyoagiza Waisraeli milele.


Walitoa vilevile sadaka za kawaida ambazo ziliteketezwa nzima, sadaka zilizotolewa wakati wa sikukuu ya mwandamo wa mwezi na katika sikukuu nyingine zote alizoagiza Yawe. Vilevile walitoa sadaka zote za mapenzi.


Kisha, viongozi wa watu wakakaa katika Yerusalema; watu wengine wote, wakapiga kura kati ya kila jamaa kumi kwa kuchagua jamaa moja itakayokaa katika Yerusalema, muji mutakatifu. Jamaa zingine tisa zikakaa katika miji yao mingine.


Nikaagiza matoleo ya kuni kufanyika katika wakati unaopaswa na malimbuko wakati wake. Ee Mungu wangu, unikumbuke kwa ajili ya haya yote na unijalie mema.


Kura inakomesha ubishi; inaamua kati ya wakubwa wanaopingana.


Kuni zote za Lebanoni na nyama wake wote havitoshi kwa sadaka ya kuteketezwa mbele yake.


Twaa unga laini, kilo kumi na mbili na kupika mikate kumi na miwili.


Mikate hiyo itapangwa kwa mistari miwili juu ya meza ya zahabu safi, kila mustari mikate sita.


Uwaamuru Waisraeli maneno haya: Ninyi mutanitolea kwa wakati wake sadaka zinazotakiwa: vyakula vya kuteketezwa kwa moto, vyenye harufu nzuri ya kupendeza.


Halafu wakapiga kura, na kura ikamwangukia Matia. Naye akaongezwa katika kundi la wale mitume kumi na mumoja.


Lakini kutokea siku hiyo, Yoshua akawafanya hao kuwa wakata - kuni na wachota - maji kwa ajili ya Waisraeli wote na kwa ajili ya mazabahu ya Yawe, popote pale Yawe alipochagua mpaka hivi leo.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ