Nahumu 3:4 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
4 Ninawe! Wewe umekuwa kama kahaba. Umewashawishi watu, ewe binti wa uchawi, uliyeyafanya mataifa kuwa watumwa kwa ukahaba wako, na watu wa mataifa kwa uchawi wako.
Sasa, basi, sikiliza, ewe mupenda raha, wewe unayezani kuwa katika usalama, na kujisemesha: Mimi ndiye. Hakuna mwingine isipokuwa mimi. Sitakuwa mujane hata kidogo, wala sitakufiwa na watoto wangu.
Haya yote mawili yatakupata kwa rafla katika siku moja: kupoteza watoto wako na kuwa mujane, ijapokuwa una wingi wa uchawi wako, na nguvu nyingi za uganga wako.
Mwangaza wa taa hautaonekana tena ndani yako. Na hakutasikilika tena kelele la wenye kuoa au kuolewa. Itakutokea vile kwa sababu wachuuzi wako walikuwa wenye uwezo mukubwa katika dunia, nawe umewadanganya watu wote kwa njia ya vitendo vyako vya uchawi.”
Wafalme wa dunia waliozini nao na kujifurahisha pamoja nao wataulilia na kuufanyia kilio wakati watakapoona moshi wa moto utakaouteketeza ukipanda juu.