Ni nani aliyewatia Waisraeli katika mikono ya waadui zao? Nani aliyewaacha wanyanganywe mali zao? Ni Yawe ambaye tumemukosea! Wazee wetu walikataa kuzifuata njia zake, wala hawakuzitii amri zake.
Basi lile pango la simba limekuwa namna gani, lile lililokuwa maficho ya simba wakali? Ile nafasi ya simba imekuwa namna gani, nafasi ya wana-simba ambayo hakuna aliyeweza kuwashitua?
Simba dume amewararulia watoto wake nyama ya kutosha, akiwakamatia simba dike nyama zao; ameyajaza mapango yake na nyama, na makao yake vipande vya nyama.