18 Wana wa Noa waliotoka katika chombo walikuwa Semu, Hamu na Yafeti. Hamu alikuwa baba ya Kanana.
Nyuma ya mafuriko ya maji, Semu, Hamu na Yafeti, wana wa Noa, walipata watoto wanaume na wanawake. Hawa ndio wazao wao:
Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misiraimu, Puti na Kanana.
Kisha Noa kutimiza umri wa miaka mia tano, akazaa Semu na Hamu na Yafeti.
Mungu akamwambia Noa: “Hiki ndicho kitambulisho cha agano ambalo nimesimamisha na viumbe vyote vyenye uzima katika dunia.”
Lakini Semu na Yafeti wakatwaa nguo, wakaiweka juu ya mabega yao, wakakwenda kinyumenyume na kufunika uchi wa baba yao. Waliangalia pembeni, wala hawakuuona uchi wa baba yao.