Nitafanya kama nilivyofanya wakati wa Noa. Wakati ule niliapa kwamba sitaifunika tena dunia kwa mafuriko ya maji. Basi sasa ninaapa kwamba sitakukasirikia tena wala sitakukaripia tena.
Lakini kwa nguvu ya neno lile lile, mbingu na dunia za sasa zimewekwa akiba kwa kuteketezwa kwa moto. Zinalindwa kwa ajili ya Siku ile ambayo watu wabaya watahukumiwa na kuangamizwa.