Mungu akaangamiza kila kiumbe kilichokuwa na pumzi ya uzima katika dunia: wanadamu, nyama, viumbe vinavyotambaa na ndege wa anga. Vyote viliangamizwa katika dunia. Noa tu ndiye aliyebaki na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya chombo.
Ondoa vilevile viumbe vyote vyenye uzima vya kila aina vilivyokuwa pamoja nawe, ndege na nyama na kila kiumbe kinachotambaa, vipate kuzaa kwa wingi katika dunia, viongezeke na kuenea kila pahali katika dunia.”
Roho zile ni za watu walioasi Mungu zamani za kale alipowavumilia katika siku Noa alipotengeneza chombo kikubwa. Ni watu wanane tu ndio waliingia ndani ya chombo na kuokolewa katika maji.