Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Mwanzo 7:23 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

23 Mungu akaangamiza kila kiumbe kilichokuwa na pumzi ya uzima katika dunia: wanadamu, nyama, viumbe vinavyotambaa na ndege wa anga. Vyote viliangamizwa katika dunia. Noa tu ndiye aliyebaki na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya chombo.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Mwanzo 7:23
21 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Nitaleta mafuriko ya maji kwa kuangamiza viumbe vyote vyenye uzima katika dunia. Kila kiumbe chenye uzima katika dunia kitakufa.


Basi, Noa akatoka katika chombo pamoja na wana wake na muke wake pamoja na wake za wana wake.


Atakuokoa mara sita toka katika magumu; hata mara saba hasara haitakugusa.


Ukikaa chini ya ulinzi wa Mungu Mukubwa, ukiishi chini ya kivuli cha Mungu Mwenye Nguvu,


Kama watu elfu wakianguka pembeni yako, hata elfu kumi karibu yako, hasara haitakupata.


Utajiri haufai kitu siku ya kasirani, lakini haki inaokoa kutoka kifo.


Halafu hawa watakwenda kwenye nafasi watakapoazibiwa kwa milele, lakini wenye haki wataingia kwenye uzima wa milele.”


Kwa njia ya imani, Noa alionywa na Mungu juu ya mambo yatakayotokea, yale aliyokuwa hajayaona bado. Yeye alimutii Mungu na kujenga chombo kwa kujiokoa yeye mwenyewe pamoja na jamaa yake. Kutokana na hayo yote akahukumu dunia na kupokea haki inayopatikana kwa njia ya imani.


Roho zile ni za watu walioasi Mungu zamani za kale alipowavumilia katika siku Noa alipotengeneza chombo kikubwa. Ni watu wanane tu ndio waliingia ndani ya chombo na kuokolewa katika maji.


Mungu hakuhurumia dunia ya zamani, lakini alimulinda Noa, muhubiri wa haki, pamoja na watu wengine saba alipoleta mafuriko ya maji juu ya dunia ile ya waovu.


Basi, ni kusema kwamba Bwana anajua namna ya kuwaokoa wenye kumwogopa katika majaribu. Lakini anangojea kuwaazibu watu wabaya kwa Siku ile ya hukumu.


Vilevile kufuatana na ile, dunia ya zamani iliangamizwa kwa mafuriko ya maji.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ