Mwanzo 7:2 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
2 Utwae pamoja nawe nyama wote wanaohesabiwa kuwa safi, dume saba na dike saba ya kila aina. Lakini nyama wanaohesabiwa kuwa wachafu, utwae dume na dike ya kila aina.
Noa akamujengea Yawe mazabahu, akatwaa mumoja katika kila aina ya nyama wanaohesabiwa kuwa safi na ndege anayehesabiwa kuwa safi, akamutolea Mungu sadaka za kuteketezwa kwa moto juu ya mazabahu.
Makuhani watafundisha taifa langu kupambanua vitu vinavyokuwa vitakatifu na visivyokuwa vitakatifu, na kuwajulisha tofauti kati ya vitu vinavyokuwa vichafu na visivyokuwa vichafu.