Kisha, wao watamwomba mungu wao, nami nitamwomba Yawe. Mungu atakayejibu kwa kuleta moto, yule ndiye Mungu wa kweli.” Na pale watu wote wakasema: “Sawa!”
Kisha Daudi akamujengea Yawe mazabahu pahali pale na kumutolea sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani. Akamwomba Yawe, naye akakubali maombi yake kwa kuleta moto kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka kwenye mazabahu.
Solomono alipomaliza maombi yake, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuchoma sadaka na sadaka za kuteketeza kwa moto zilizotolewa, kisha utukufu wa Yawe ukajaza nyumba.
Yawe akawasha moto ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa na mafuta yaliyokuwa juu ya mazabahu. Watu wote walipoona huo moto wakapiga vigelegele na kuinama uso mpaka chini.
Lakini wazaliwa wa kwanza wa ngombe, kondoo au mbuzi wasikombolewe; hao ni watakatifu. Damu yao utainyunyizia mazabahu na mafuta yao utayateketeza kuwa sadaka ya kuteketezwa ambayo ni harufu nzuri inayonipendeza mimi Yawe.
Kwa njia ya imani, Abeli alimutolea Mungu sadaka nzuri zaidi kuliko ile ya Kaina. Kwa ajili ya imani yake alihesabiwa na Mungu kuwa mwenye haki, kwa maana Mungu mwenyewe alikubali sadaka zake. Na kwa imani ile, ingawa Abeli amekwisha kufa, angali anasema.
Wakaaji wote wa dunia watamwabudu, ndio wale wote ambao tangia kuumbwa kwa dunia, majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo aliyechinjwa.
Malaika wa Yawe akanyoosha fimbo yake, akagusa nyama na mikate kwa incha ya fimbo. Kwa rafla, moto ukatoka ndani ya jiwe, ukateketeza nyama na mikate. Mara moja malaika wa Yawe akatoweka mbele yake.
Halafu Samweli akamwambia: “Unazani kwamba Yawe anapendelea zaidi sadaka za kuteketezwa kwa moto na matoleo mengine, kuliko kuitii sauti yake? Hapana. Kumutii yeye ni bora kuliko matoleo na kumusikiliza kuliko kumutolea mafuta ya beberu.