Ni nani huyu anayekuja kutoka Edomu, anayefika kutoka Bosira na nguo ya madoa mekundu? Ni nani huyo aliyevaa nguo ya utukufu, anatembea kwa nguvu zake kubwa? Ni mimi Yawe ninayetangaza ushindi wangu; nami ni mwenye nguvu ya kuokoa.
Saulo alipokwisha kuwa mufalme wa Waisraeli, alipigana na waadui zake wote kila upande: Wamoabu, Waamoni, Waedomu, wafalme wa Zoba na Wafilistini. Kila mara alipopigana vita, alishinda.