Lakini siku hiyohiyo Labani akakwenda akatenga beberu wote wenye mistari na madoadoa, mbuzi wote dike waliokuwa na madoadoa na matakamataka, kila nyama aliyekuwa na weupe kwenye mwili wake, na kila kondoo mweusi, akawaweka chini ya ulinzi wa wana wake.